Friday, October 29, 2010

JAMANI RESHMAIL---07

"JAMANI RESHMAIL-07"

by George Mosenya on Monday, October 25, 2010 at 8:51pm
Hakuwa hata na chembe ya utani Reshmail wa watu,majira ya saa moja asubuh tayari alikuwa kwenye gari la KIMOTCO ninalotoka Arusha kwenda Musoma kwa kupitia Serengeti,kitu kinachoitwa hofu moyoni hakikuwepo hata kwa mbali,ndan ya kipoch chake kidogo alikuwa na pesa taslimu za kitanzania shiling laki mbili zikisindikizwa na kadi ya viza ya CRDB iliyokuwa na uwezo wa kutoa shiling laki tano kwa siku mara nne yaani milioni mbili zilikuwa zimehfadhiwa katika acount yake ya akiba.Mamaa wa shughuli (Eveline) alikuwa pembeni ya Reshmail,hofu kwake haikuwepo wala hakuiwaza tayari alikuwa mzoefu wa mambn hayo."Eveline yani akili ndo inakuja sasa hv eti kwa nin tusingepanda ndege dah! gari linaenda taratibu hlo jaman" alilalama Reshmail kwa wananch wa kawaida waliomsikia walidhan ni mashauzi ya watoto wa kike "Mh? shoga ulivyokuwa na hamu ungekumbuka hayo,tutafika weye acha papara"
Gari lilizidi kuchanja mbuga za ngorongoro kwa kasi ya kawaida hadi majira ya saa saba tairi chakavu za gari hli zilikuwa tayari kwenye mbuga za serengeti,Resh alikuwa macho anatazama safari inavyokwenda huku akihesabu masaa yanavyokatika kwa kasi huku mwisho wa safari ukiwa haufiki.Eve yeye alikuwa ameuchapa usingzi huku akiwa amejifunika uso wake kwa kofia yake nyeus ambayo vumbi ilikuwa imeibadili rang yake na kuwa ya ugoro.(Brown).
"Eve eve eve,amka uone wewe" Resh alikuwa anamwamsha kwa fujo."Angalia hii sms imeingia sasa hv" "Resh mazako kaja unatafutwa uko wap?" jasho jembamba likaanza kumtoka resh lakin Eve hakushtuka sana.Walikuwa wametumiwa ujumbe mfup na mmoja wa viranja."Eve tumeisha tumeisha"

* * * * * * * *

Ulikuwa mshikemshke wa ghafla pale shulen mwalimu aliamuru kila mmoja aje mstarini hata kama ni mgonjwa,viranja walitii amri na kuita wanafunz wote kwa haraka hakuna hata mwanafunz mmoja aliyebk ndan ya bwen.
Wakiwa hawajui nini kinachoendelea mwalimu wa zamu aliyeitwa Mwl.Chipeta alikuwa mbele ya wanafunzi waliokuwa kimya kumsikiliza yeye.Kabla sijatoa tangazo hili,ni nan anatambua mwanafunz ambaye hayupo? (Kimya) "Nani anaumwa na amepewa ruhusa?" (Kimya) "Kwa hyo wote mpo?" (Ndiooo) "Haya mchepuo wa H.G.E wote pita mbele" aliamuru mwalim Chipeta na kwa haraka wakaanza kujongea mbele."Mamaaaaa," ghafla kelele ilisikika kuna mwanafunzi aliyekuwa mgonjwa alikuwa ameanguka chn kwa sababu ya kizunguzungu.Ustaarab ukatoweka pale ghafla kila mwanafunzi akawa anasema lake,mara hv mara vile. Hata mwalimu Chipeta alitimua mbio kuelekea kwenye tukio.
Ni wakat huohuo Joyce ambaye alikuwa kiranja alipata mwanya wa kutuma ujumbe kwa Reshmail kumpa taarifa.

* * * * *

No comments:

Post a Comment