Friday, October 29, 2010

JAMANI RESHMAIL---06

"JAMANI RESHMAIL-06"

by George Mosenya on Thursday, October 21, 2010 at 3:26am
Majukumu ya hapa na pale yalikuwa yamembana sana Bi.Gaudensia ambaye ni mama yake na Reshmail,pia uwepo wa mumewe katika himaya yake ilimnyima kabisa raha mama huyu na alikuwa anakosa nafasi ya kwenda Arusha mara kwa mara kufurah na mwanaye jambo ambalo lilimtesa kwa takribani mwezi mmoja na nusu.Vipindi vya bunge vilipoanza tena ndio hapo nafasi ilipatikana tena,kwa muda wote ambao alikuwa jijin dar-es-salaam Bi.Gaude alikuwa akiwasiliana na mwanae karibia kila siku kwa njia ya simu,alijua ni jinsi gan hata mwanae huyo alivyo'm-mis' hvyo aliamua kumfanyia 'surprise' ya kwenda huko Arusha shuleni bila kumwambia ili kuinogesha furaha yao ambayo ilikuwa inakamilika kitandan."Baba Resh mie kesho naenda kumsabah mwanetu,lakin hata simwambii nataka ashtukie tu,mama huyo"
"Atashangaa kweli,msalimie sana mwambie nitakuja kumsalimia bunge likimalizika" "Haya,zimefika"

* * * * * *

Penzi la ku-chat katika mtandao wa facebook lilikuwa limemchanganya sana Reshmail wa watu,Adam hakuwa nyuma kumpa maneno matamu ya hapa na pale ambayo kamwe alikuwa hajawah kuyasikia masikion mwake,Eve mwenyewe alimshangaa huyu shoga yake lakin hakuwa nyuma kumpiga tafu katika mpango mzima wa kumtia Adam majaribuni ndio maana alimshawish Resh kupga picha mbaya ambazo mwanaume yeyote akiziangalia lazima ajiulize mara mbilimbili kuhusu urembo asilia wa binti yule.
"Mi nipo peke yangu siku hizi rum-mate wangu ameenda kwao babake anaumwa" "Don't tell me kuwa unalala mwenyewe"
"Nitafanyaje sasa na wewe upo mbali?"
"ooh! my ghosh! assume nipo hapo"
"Aah,nitajiumiza bure tu mpenzi wangu"
"Anarudi lini kwani?"
"Mh! amesema atatumia kama wiki mbili hv,njoo basi unipe 'kampan' kiaina"
Yalikuwa mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Adam na Reshmail yaliyokatishwa na na mlio wa 'low battery' katika simu ya Reshmail "Baby boy tutaongea kesho,pole sana na ninakupenda sana" alimaliza resh na simu ikawa imezima.
"Eveline nataka kwenda Mwanza" asubuh ya siku iliyofuata Resh alimwambia Eve."He! makubwa haya,imekuwaje kwan shoga" aliduwaa."Mi sijui lakin nataka kwenda tu" alisema reshmail "Haya lini wataka kwenda?" "Hata kesho mi naenda tu" "Mh! sikuwez haya jiandae kutoroka coz ruhusa hapa kupata sahau" "Vyovyote poa ninachotaka ni kuondoka na kwenda Mwanza that's all" alijibu kijasiri Resh hali iliyomduwaza eveline.

* * * * * *

"Reshmail hayupo? mbona jana alikuwa hapa ofisin?" mwalimu wa zamu alikuwa anamuuliza mwanafunzi aliyeagzwa kumuita Reshmail baada ya mama yake kuwa amefika,"Hata mi sijui mwalimu"
"Hapana sio jambo la kawaida reshmail kutokuwa mazingira ya shule tena jumatatu! hebu mwambie time-keeper agonge kengere mara moja" aliamrisha mwalimu.

No comments:

Post a Comment