Friday, October 29, 2010

JAMANI RESHMAIL---01

Mwanza,Tanzania.

"Reshmail Msuruli want to be your friend.'confirm' 'ignore' ulikuwa ni ujumbe ambao macho yangu yalikutana nao nilipofungua mtandao wa facebook,sikumbuki kama nilijifikiria mara mbili kwan niliona kama jambo la kawaida sana kukutana na 'notifications kama hzo,na mara zote neno confirm lilipata fursa ya kutumika.hivyohivyo hata kwa reshmail nilifanya hvyo."You and reshmail are now friends" ndio ujumbe ulionisindikiza baada ya ku'confirm'..
* * * * *
Ni kijana mtanashati niliyebahatika kukutana nae pale chuoni saint.augustine mwanza,alijipenda kuanzia ndan ya chumba chake hadi mwilini mwake,ilikuwa ni nadra sana kumfumania akiwa amevaa nguo aliyoivaa jana,bila kumnyima haki yake nasema alikuwa anapendeza kila siku,macho yangu ya kipelelezi na camera zangu za kipaparazi kamwe hazikufanikiwa kumjua aliyekuwa ubavu wa bwana huyu 'MPENZI' ukipenda waweza kuniita mbeya lakin ukiniita hvyo basi waite wote pale chuon kwani walipenda kumpeleleza wamjue na kamwe hawakufanikiwa.
Binadamu hatuna dogo watu washaanza kusema eti huenda jamaa ana matatizo 'downstairs' mh! mi sikuwa mmoja wao lakin nilijiuliza pia kulikon?? makala zilizokuwa zinaandikwa na gazeti la chuon ndo zilinizonivuta zaid kutaka na mimi siku moja kuandika katika gazeti hilo lililokosa mvuto siku za hv karibuni.Taratibu nilijenga mazoea na hatimaye nikafanikiwa kumzoea "THE MOST WANTED" uchesh wangu ndo uliomvutia zaidi kupenda kuwa karibu nam,haukupita mwezi mzima nikawa nina uwezo wa kuanza kazi yangu,ni mimi na Adam Michael kwenye meza moja chumban kwangu ananipa hadith yake ya mapenz.
"Aah!! jamani RESHMAIL..." yangu masikio na macho nikaanza kusikiliza kwa makini.
@ @ @ @ @

kwa nin adam anasema hvyo?

No comments:

Post a Comment