Friday, October 29, 2010

JAMANI RESHMAIL---02

JAMANI RESHMAIL-02

by George Mosenya on Thursday, October 21, 2010 at 3:23am
>> Hadi anafika mwaka wa pili kimasomo chuoni S.T Augustine kitivo cha sheria Adam aliitumia simu yake kwa ajili ya kupiga,kutuma sms na kupokea ni hayo tu na kwa upande wa pili alipenda sana kucheza game ya kwenye simu.
Alikuwa ni Hughorito Hamada ama maarufu kama 'HUHA'.hakuwa tu rafiki yake adam bali pia alikuwa ni 'roomate' na classmate wangu pale chuon,ni huyu aliyemuingza adam katika ulimwengu ambao hatausahau kamwe,tabia yake ya kupenda kuazima simu ya Adam aina ya Nokia Expres music kwa dhumun la kuchat ndio ilimshawish adam naye kuanza kujiuliza kulikoni hasahasa alipokuwa anamwona Huha akicheka mwenyewe kila anapokuwa anachat,"Mh! we jamaa yangu chzi kwel yan unacheka na watu usiowaona" Adam alimkebeh Huha alipokuwa anacheka na simu yake "Kwani we ukiwa unaota unaongea huwa kuna watu mbele yako?" Huha alijibu mashambulizi na adam akabaki kimya na taulo lake kiunoni akaenda bafuni kuoga,"Mwanangu nimekuunga na wewe password yako ni..,.." hata kabla Huha hajamaliza adam akamkatisha "Nini? huo upumbavu wako sitafanya kamwe bro" ..."Hv kwan inakuwaje huo upuuzi" Adam akajikuta anauliza baada ya kuwa amevaa nguo zake "Hii kitu inaitwa FACEBOOK,yan adam ukijiunga wewe hutoki na utakuwa nayo bize kweli" Adam alisikiliza kwa makin japo alijidai kufanya dharau machon,Huha hakujali aliendelea kutoa somo had Adam akapata mwanga,"Mh. Sidhan kama itanivutia bt i wil try". Alijisemea adam wakat anachukua simu yake.

###### ########## ######
Tabia ya Adam ilikuwa imebadilika ghafla ni Adam na facebook,facebook na yeye,iwe barabaran,club,lecture room,hostel yani kasoro mskitini tu ndio Adam aliweza kuhfadh simu yake.Sio Huha wala rafiki yake yeyote aliyejua nini zaid ya facebuk kimemuathiri adam wa watu.Hakumuazima tena Huha simu,hakutaka mazoea na wasichana ni yeye na simu yake tu!! "Adam mbona washkaji wanalalamika eti wanakuomba urafiki facebook unachomoa? siku moja Huha aliamua kumuuliza Adam baada ya kuona tabia yake imekuwa ya ajabu mno kupindukia."Sitaki that's all". Ndio jibu fup alilopewa.kisha adam akajiondokea.Huha akabaki ameduwaa asijue la kufanya,mara ghafla adam akarudi tena "Huha naomba ukamwambie Halima simtaki,usiniulize kwa nini mwambie SIMTAKI!" adam alimwambia Huha kana kwamba alimfumania huyo halima.
Mpenz msomaj Halima alikuwa binti matata pale chuon kwa kipind kile,Adam ndo alipata fursa ya kuangukia penz lake,penz lao chuo kizima walifahamu,gari ya Halima ilikuwa kama ya Adam..chumba cha Cha Halima kilipambwa picha na kad za Adam lait na Adam angekuwa anakaa peke yake basi hata yeye chumba chake kingekuwa had na nguo za ndan za Halima pamoja na pedi bas tu alikuwa anakaa na Huha.
Huha alibak mdomo waz akijiuliza ni Adam au kivuli chake kinaongea.Alikuwa Adam sio kivuli.....

nin kimemsibu adam?
Reshmail ni nan!

No comments:

Post a Comment